Joel Lwaga Bila Bila Lyrics
Nikitazama nilikotoka Hapa nilipo ninapokwenda Ninagundua
Ingekuwa ni nguvu zangu ningeshachoka nisingeweza
Sio kweli kwamba tu ku-hustle na kupambana ndio vimenitoa
Juhudi haizidi kudra siwezi sema babu hakujituma
Niliitwa ndugu lawama
Mfano wa waliokwama
Mtu asiye na maana wa kuchekwa kudharauliwa
Ila Mungu ana maguvu bwana Leo nikipita wanaitana sa ngoja nami niwaite niwape siri ukweli ni kwamba
Bila Mungu mimi bila bila
Hamna kitu yani Zero bila
Bila Mungu mimi bila bila
Sina una ujanja yani zero bila
Mmmh yani kama Meli isiyo na nahodha
Kama bunge lisilo na hoja
Mi ni debe tupu bila ya Mola
Msidanganyike nje mnanvyoniona
Sina mzizi wala Mlozi
Nina mtetezi tena yu Hai
Ye ndo siri ya mi kunawiri
Bila Ye mi chali na sifurukiti
Niliitwa ndugu lawama
Mfano wa waliokwama
Mtu asiye na maana wa kuchekwa kudharauliwa
Ila Mungu ana maguvu bwana Leo nikipita wanaitana sa ngoja nami niwaite niwape siri ukweli ni kwamba
Bila Mungu mimi bila bila
Hamna kitu yani Zero bila
Bila Mungu mimi bila bila
Sina una ujanja yani zero bila