Marioo 2025 Lyrics (feat. Stans)
Babe niposti
Kwani me si mali yako
Unamuogopa nani
Ai wewe eeh!
Babe nichumu
Kwani me si mali yako ooh
Unamuhofia nani
Aiih wewe
Me naona raha
Kama tunawakera ah
Na bila hata kuwagusa
Bila hata kuwasema
Me naona raha
Kama tunawaboa aah
Bila hata kuwaomba
Bila hata kuwagasiii ah
Mungu kaumba dunia ina watu na viatu ah
Kaumba dunia ina vitu na vituko oh
Mungu kaumba dunia ina watu na viatu ouh
Ila si tunavyopendana wataachana wao tunadunda mpaka
Mbili ishirini na tano, mbili ishirini na sita
Mbili ishirini na saba, ooh mbili ishirini na nane
Tunadunda mpaka mbili ishirini na tisa ooh mbili thelathini
Ooh ila si tunavyopenda wataachana wao oh
Babe naomba nifanye
Babe naomba nifanye
Nifanye niweke daima mpaka mwisho
Babe naomba niweke
Babe naomba niweke eeh
Ndani ya moyo wako daima
Wale wote wanaojifanya pweza
Wa kutabiri penzi
Mwaka huu tuwachinje
Tunywe chuzi la kuongea nguvu (Aah)
Wale wote wambea, wambea
Watie chumvi penzi
Midomo tuwafumbe
Tupendane waishiwe nguvu (Aah)
Mungu kaumba dunia ina watu na viatu ah
Ila si tunavyopendana wataachana wao
Tunadunda mpaka
Mbili ishirini na tano, mbili ishirini na sita
Mbili ishirini na saba, ooh mbili ishirini na nane
Tunadunda mpaka mbili ishirini na tisa ooh mbili thelathini
Ooh ila si tunavyopenda wataachana wao oh